FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
CHONDE CHONDE !! WATANZANIA PUNGUZENI KUZAA.. |
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.. Rais Samia Suluhu
Hassan amewataka wananchi wake kupunguza kasi ya kuzaa, kutokana ongezeko la
idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kwa sasa.
Ametoa kauli hiyo
baada ya kushtushwa na taarifa aliyopewa kuhusu idadi kubwa ya watoto
wanaozaliwa kwa mwezi.
Akizungumza na
wananchi hao wa Bukombe, magharibi mwa Tanzania, Rais Samia alitoa kauli hiyo
akiwata wapunguze kasi.
''Jana nimesimama
Buselesele pale, nikaambiwa kituo kimoja (cha afya) kinazalisha watoto 1,000
kwa mwezi, sasa hayo madarasa baada ya miaka 3 ni mangapi?, kama ni vituo vya
afya ni vingapi? tani za chakula ni ngapi,? kidogo speed (kasi) tupunguze
kidogo'', alisema rais Samia.
Rais Samia aliyasema
hayo wakati wa ziara yake ya kawaida ya kiserikali ndani ya nchi hiyo.
Katika kiwango cha sasa
cha ukuaji wa idadi ya watu, idadi ya watu huongezeka mara mbili katika kipindi
cha miaka 25.
Wakati ikisubiriwa
taarifa rasmi ya sensa ya watu iliyofanyika mwaka huu, nchi hiyo inakadiriwa
kuwa na watu zaidi ya milioni 60, kutoka kadirio la watu milioni12.5, katika
miaka ya 1960. |