FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
Balozi Ali Karume amulikwa na kurunzi ya maadili ya CCM. |
Mwanasiasa na mwana diplomasia
nguli hapa nchini, Balozi Ali Karume ambaye pia ni mtoto wa mwasisi wa
mapinduzi matukufu ya Zanzibar Rais Abeid Aman Karume katika siku za hivi
karibuni amejikuta matatani kutokana na kauli zake zenye ukakasi dhidi ya chama
cha CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ujumla wake.
Hatua hiyo inatokana
na onyo alilopewa na kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Jimbo la Tunguu,
Mkoa wa Kusini Unguja iliyokutana Juni 15, 2023.
Balozi Karume aliwekwa
“kiti moto” na kamati ya maadili ya jimbo hilo kutokana na kauli zake
alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii akikituhumu chama kuwa hakijawahi
kushinda kihalali kisiwani humo na kumkosoa hadharani Rais Hussein Mwinyi
kuhusu sera zake za kukodisha visiwa.
Pia alipinga utaratibu
wa wananchi wa Kilimani kuondolewa kujenga ukumbi wa kimataifa na ujenzi wa
uwanja wa Amani akidai vinakiuka utaratibu.
Juni 11, katika moja
ya mikutano yake, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi
aliiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia makada wanaokwenda kinyume na
taratibu huku akihoji kwanini bado wako ndani ya chama.
“Wakati umefika kwa
kamati ya maadili kufanya kazi yake, una sababu gani ya kubaki kwenye chama
hiki, ikiwa hupendi chama ondoka! Nenda ukaseme hayo maneno ukiwa nje ya chama,
unahoji hata ushindi wa CCM!” aliwaambia wafuasi bila kumtaja mtu.
Kwa mujibu wa barua
ambayo Mwananchi limeiona iliyosainiwa na Katibu wa CCM jimbo la Tunguu,
Sharifa Maabadi Othman, bila kutaja muda, inaeleza chama kumpa onyo hilo kwa ukiukwaji
wa maadili.
“Pamoja na mambo
mengine kikao kilipokea taarifa kutoka kamati ya maadili ya jimbo kuhusu
mahojiano yaliyofanyika juu ya Balozi Ali Abeid Karume na kamati ya maadili ya
jimbo, baada ya kukiri makosa yake mbele ya kikao hicho, aliomba msamaha, hivyo
basi kikao kimeamua kukupa onyo kwa kukiuka maadili ya chama chetu,” inaeleza
sehemu ya barua hiyo.
Hata hivyo, alipo
ulizwa katibu huyo Sharifa kuhusu hatua hiyo, licha ya kusema hawezi kuzungumza
chochote kwa sababu yaliyofanyika ni vikao vya ndani, alikiri barua hiyo ni
halali.
katika kuthibitisha
kuwa kuna msuguano wa kimawasiliano kati ya Balozi Ali Karume na uongozi wa
chama jimboni, alisema naye ameona barua hiyo kwenye mtandao wa kijamii, na akasema
ikimfikia atatii maadili ya chama.
Balozi Karume
alihojiwa na kamati ya maadili ya tawi la Mwera, kamati ya maadili ya Jimbo la
Tunguu na kamati ya maadili ya Wilaya ya Kati.
Barua aliyopewa Karume
ni kwa mujibu wa kanunzi za uongozi na maadili za CCM na jumuiya yake toleo la
mwka 2021 ibara ya (8) kifungu kidogo (a) (ii).
Nakala ya barua hiyo
ilikwenda kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kati na Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini
Unguja.
Kutokana na kanuni
hiyo mwanachama anayekiuka maadili ya chama anapewa onyo, onyo kali au
kufukuzwa uanachama huku kukiwa na muda maalumu wa uangalizi kuanzia miezi
mitatu, sita na mwaka mmoja.
Mmoja wa watu wa ndani
ya chama hicho ambaye hakutaka kutajwa alisema iwapo kikipita kipindi cha
uangalizi bila kuonyesha mabadiliko, wilaya itatoa mapendekezo kwenda ngazi ya
mkoa kwa hatua zaidi.
Mapendekeo hayo
yanaweza kuwa kumfukuza uanachama kiongozi huyo.
Akizungumza na gazeti
hili mchambuzi wa masuala ya kisiasa Zanzibar, Ali Makame alisema hatua
iliyochokuliwa ni sawa kwa sababu lengo la kila chama ni kuishika dola, lakini
kuna taratibu za kufuata katika kuzungumza.
“Ukiangalia huyu ni
mtoto wa muasisi wa taifa hili na chama chake, kwa hiyo anajua mengi, madhaifu
na mazuri ya chama, lakini kutoka hadharani na kuanza kusema vile si uungwana,
kama unapinga tumia utaratibu wa chama unapotoka nje unakuwa utovu wa nidhamu,”
alisema
Hata hivyo, alisema
hatua zilizochukuliwa na chama hicho ni jambo la kujifunza hasa kwa watu
wengine kwa sababu linaweza kuwagawa wanachama na viongozi, hivyo kuwaondoa
kwenye lengo la chama kama kikundi chenye dhamira moja.
Taarifa hii ni kwa
hisani ya ; Jesse Mikofu Mwandishi wa Habari - Mwananchi |