FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
Apiga “Hatrik” harusini !! |
Bwana
Athuman Yengayenga, mkazi wa Shanwe, Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,
Tanzania, awashangaza wengi baada ya kuamua kuoa wanawake watatu kwa mpigo,
tukio lililomulikwa na vyombo vingi vya habari hapa nchini. Alipo
hojiwa ni sababu ipi hasa iliyo mpa hamasa ya kufaya hayo yote, alijibu kwa
haraka kana kwamba alitarajia kuulizwa swali hilo. “naam ! lengo langu lilikuwa
kuoa wanawake wanne kabisa, ili nifunge haya mahesabu ya kuoa” aliongea kwa
msisitizo.. Huu
msukumo wa kuoa ulikuja baada ya kuachwa na mke wangu kipenzi aliye niachia
maumivu makubwa moyoni na kuniathiri sana “kisaikolojia”. Na kila nilipo fikiri habari ya kuoa tena niliona mwanamke mmoja hatonitosheleza, ndo nikaja na wazo la wanne, lakini Mwenyezi Mungu Subhuhanna bhuh’ wat-Allah akanijaalia watatu Alhamdulilakh ! nashukuru, na inshaAllah !! ibada ya kumilisha wanne ntaifanya mbele ya safari, kunako uzima. Na
sababu nyingine muhimu ya kubeba watatu kwa mpigo, ni kwamba hata likitokea la
kutokea hawawezi ondoka wote ghafla, kuna watakao baki kunifariji na madhila ya
upweke, hivyo kuninusuru na hatia ya kujichukulia sheria mkononi. Watoto hao warembo na wabichi kabisa
Fatuma Rafaeli, Asha Pius na Mariam John ambao ni wana ndoa halali wa huyu
mwamba Bwana Athuman
Yengayenga, waliongea kwa kauli moja kwamba “wivu ni suna katika maisha ya
ukewenza” na wamejiandaa kikamilifu katika hilo kwa kumuomba Allah! awazidishie upendo na ushirikiano baina yeo
kwa ajiri ya kumtunza na kumfurahisha mume wao kipenzi. Kwao kumuangali Mume
jambo la msingi katika maisha yao kuliko kitu chochote, na kiimani hii ni ibada
pia kwetu. “Bado hatujakamilika, tunamsubiri wanne
kukamilisha Sunah !” alisikika Bi. Fatuma akiwa kama bi mkubwa huku akitabasamu
na kuweka vizuri shera lake la harusi. Hata hivyo imebainika kuwa Bwana Athuman Yengayenga ametokea katika ukoo wa ndoa za mitala. Baba yake alikuwa akiishi na wake wengi. |