FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
FEISAL SALUM ABDALLAH (Fey Toto) NI MCHEZAJI MWENYE KIPAJI CHA MPIRA WA KUZALIWA..
- Simon Kimanga
- 2024-03-23
Buriani Mh. Edward Lowassa. |
Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk.Alex Geaz MALASUSA ametoa
agizo kwa wachungaji kutopokea miili ya watu waliofariki ambao hawakuwa
wakihudhuria ibada kanisani wala kushiriki ibada za nyumbakwanyumba wakati wa
uhai wao.
Askofu amefafanua kuwa
katazo hilo lina lenga katika kuheshimu misimamo waliyokuwa nayo wakati wa uhai
wao. “Ukileta mwili kanisani wakati mhusika alipokuwa hai alikuwa na uwezo wa
kukubali au kukataa kuhudhuria ibada ni kuuonea mwili huo, “amesema Dk.
Malasusa.
Hayo ameyasema siku ya
Februari 14,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa ibada maalumu ya kuaga mwili wa
Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa aliyefariki Februari 10 mwaka huu
wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete(JKCI)iliyofanyika katika Usharika wa Azania Front na kuhudhuliwa na
viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Amesema Lowassa
alikuwa mpenda ibada wakati alipokuwa na uwezo wa kwenda kanisani alifanya
hivyo kila wakati hivyo hivyo nitoe rai kwa wananchi wote bila kujali dini zao
kutumia nyakati kama hizi kumtafakari Mungu zaidi na kujisogeza karibu na
Mungu.
Amesema Edward
alipenda ibada enzi za uhai wake ambapo hata wachungaji walioongoza ibada hapa
kanisani watashuhudia kuwa alikuwa mtu wa ibada.
Dk. Malasusa
amesisitia ukweli utabaki kuwa ukweli haijalishi wanasema nini watoto na Mke wa
Lowassa hongereni kwa kuwa na Baba ambae kila mtu anasema mazuri yake na
amegusa maisha ya waliowengi.
“Kama hujawah
kupotelewa na ndugu mzazi huwezi kuelewaa neno “pole” ulikuwa unacheka nae mna”share”
lakini leo hayupo jambo kubwa ni kumuomba Mungu akuondolee maumivu na kukutia
nguvu,”amesema.
Amesema wao
wanaomwamini Mungu duniani wanapita baada ya maisha hayo kuna maisha mengine.
“Edward anastahili maua
yake kweli kweli, alipenda ibada na namshukuru mama Regina, alikuwa naye bega
kwa bega pamoja kuwa ni mkatoliki kweli kweli lakini walihimizana kwenda ibada
Mama Regina na familia kwa ujumla niwaombe yale yote mliyotenda wakati wa uhai
wa Edward Lowassa naomba myaendeleze,” ameongeza.
Aidha amesema hakuna
ulazima katika kanisa kufungua na kuona mwili wa mwanadamu aliyefariki na sio
sheria ya kanisa au maandiko ya bibilia kufanya hivyo.
“Tuwe tunatazamana
tukiwa hai tusisubiri mtu amelala, msifikirie kwenda kuaga ni lazima ufungue mtu
umwone siyo lazima, naiopongeza familia ya Lowassa kwa kufanya hivyo na ikawe
mfano kwa wengine,” amesema.
Naye Mbunge wa zamani
wa Jimbo la Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni amesema Waziri Mkuu Mstaafu
Lowassa angeweza kuishi zaidi kama isengekuwa ajali mbalimbali za kisiasa
alizokutana nazo.
Ameeleza kuwa siasa
ilimletea mgogoro mkubwa lakini alisimama na kuacha alama na siku zote alikuwa
mtu mwenye upendo.
Amesema 2015 walianza
safari ya matumaini ambayo kote walipokwenda watanzania walionyesha matumaini
makubwa kwa sababu waliamuamini sana Lowassa kwamba ndiye kiongozi anayeweza
kuwavusha watanzania katika harakati za kuwaongoza
“Tunahitaji wazee kama
mzee Jaji Joseph Warioba amemuelezea Lowassa mwanzo mwisho uliongea kutoka
moyoni hukuongea kama mwanasiasa Lowassa alikuwa mvumilivu, “amesema Dk.
Chegeni.
Kwa upande wake Mtoto
Lowassa Fredrick Lowassa amesema muda wote alipokuwa na nguvu alikuja kanisani
na amewafundishwa hivyo kupenda kufanya ibada.
Amewashukuru viongozi
wote na wananchi wote walikuwa wanamuombea baba yao wakati akiugua hadi
anafikwa na umauti.
Waziri Mkuu Mstaafu
Hayati, Edward Lowassa anatarijia kuzikwa Februari 17 mwaka huu Ngarash Wilaya
ya Monduli.
Bwana ametoa na Bwana
Ametwaa ; Jina la Bwana YESU Lihimidiwe..
Na mwandishi:- Sophia
Kingimali.. |